Deuteronomy 3:11-13

11 a(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa
Dhiraa tisa ni sawa na mita 4.
na upana wa dhiraa nne.
Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.
Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

(Hesabu 32:1-42)

12 dKatika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake. 13 eKisha nusu ya kabila la Manase niliwapa sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani yote, ambayo ilikuwa utawala wa Ogu. (Eneo lote la Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama nchi ya Warefai.
Copyright information for SwhKC